Meli ya Azam Marine inayoitwa Azam SeaLink 1 ikiwasili katika bandari ya Visiwani Zanzibar kwa mara kwanza.
Baadhi ya wakazi wa Zanzibar wakipiga picha Meli hiyo iliyowasili Visiwani Zanzibar leo.
Mzee Said Salim  Bakheresa (mwenye nguo nyeusi) akikagua mazingira ya Meli hiyo baada ya kuwasili Bandari ya Zanzibar leo.
Sehemu ya Parking yenye uwezo wa kuingiza magari 200.
Muonekano wa ndani wa Lounge ya kumpzikia wasafiri.
Muonekano wa nje. (Picha na Omar Said wa Kampuni ya Bakheresa).
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Kampuni ya Azam Marine inayomiliki boti ziendazo kasi hapa nchini, leo imeingiza meli mpya na ya kisasa itakayochukua zaiidi ya abiria 1500 na magari 200.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Azam Marine, Bw. Hussein Mohammed Saidi, amesema leo mjini Zanzibar kuwa meli hiyo ambayo itafanya safari zake kati ya Dar es Salaam, zanzibar na Pemba itatoza nauli nafuu kwa abiria wake.
Amesema meli hiyo ambayo inatarajiwa kuanza safari zake mara baada ya kukamilisha taratibu za mamlaka mbalimbali.
Meli hiyo inayoitwa AZAM SEALINKI ni ya kisasa katika ukanda huu wa Mwambao wa nchi za Kusini na Pembe ya Afrika.
Bw. Hussein amesema Meli hiyo ambayo imetengenezwa nchini Ugiriki na inatayarishiwa eneo maalumu litakalotumika kwa kupakia na kushusha abiria na mizigo yakiwemo magari.
Amesema meli hiyo itasafiri kwa muda wa saa tatu kutoka Dar es salaam na Zanzibar na saa 4 kutoka Zanzibar na Pemba ama saa 7 kutoka dar es salaam na Pemba.
Amesema pamoja na kuwasili kwa Meli hiyo, Kampuni ya Azam pia inatarajia kuleta meli nyingine ya abiiria inayojulikana kama Kilimanjaro namba 4.
Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wa Visiwa vya zanzibar wamepongeza ujio wa meli hiyo lakini wakaitaka serikali kuendelea kudhibiti uingizwaji wa meli chakavu na kukuu ili kuepuka uwezekano wa kutokea ajali za mara kwa mara.
Bwana Rajabu Khamisi mkazi wa Pemba na Bi. Rehema Omari wa mjini Zanzibar, wamesema kuna haja ya Serikali kusimamia ukomo wa nauli ili kila mwananchi aweze kusafiri kutoka sehemu moja na nyingine kwani wamesema vipato havilingani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Safi sana Mr. Said Bakheresa wewe ndio Mwanamume. Tunahitaji watu kama wewe kwenye Nchi zetu za Tanzania na Zanzibar sio wapiga domo tu.

    Tanzania na Zanzibar bila viongozi kama Mzee Bakheresa hatutafika popote kwani Wajasiliamali ndio waleta Maendeleo.

    Tumeona uozo ulio jaa kwenye shirika la nyumba la Taifa kwa Kuingia ubia na Makampuni ya nje Kujenga Vyumba nya ghalama katikati ya jiji la Dar na Kutoza kodi ya Milioni moja mpaka milioni Tatu kwa Mwezi kwa vyumba viwili huu ni Ugonjwa kabisa.

    Mzee Bakheresa amesema atatoza Bei za Nafuu kwa kila abiria na kuwawezesha wananchi kusafiri na kufanya shughuli zao za kila siku.

    Watanzania ni Lazima tuamke na tuchague viongozi watenda kazi, hasa ambao walisha tenda kazi na zikaonekana kama Azam.

    Sasa huyu Kabwe Zitto anataka Uraisi na Hata kajawahi kutenda chochote.

    zito Hajawahi kuwa na Biashara yeyote ambayo imeshatoa hata ajira.

    Hana Shamba ambalo kisha Miliki hata Trekta moja ambalo limeajiri wakulima. Kwanini Anataka Uraisi?????

    ReplyDelete
  2. Safi sanaaaaaaa. Sasa Zanzibar wajiande kupokea wageni na magari yao....

    ReplyDelete
  3. Hongereni kwa hayo, wasiwasi wangu mkubwa ni haya;

    Tunaomba mamlaka husika iweke wazi JE! NI MPYA AU KUUKUU? IMETENGENEZWA MWAKA GANI N.K. Isijekuwa imepakwa rangi na kufanyiwa ukarabati wa kutosha.

    Tumechoka kuona maisha ya watanzania yakizidi kupotea kwa mambo ambayo yangeweza kupatiwa tiba mapema. Wakati umefika wa kuweka masharti magumu kwa wamiliki wa vyombo hivi ili kuleta vyombo bora kwa ushundani wenye manufaa na tija kwa watanzania.

    Mwananchi wa kawaida

    ReplyDelete
  4. MUNGU ATAMLIPA SSB INSHAALLAH.UKU BAKHERESSA UKU DR DAU MBELE JK NCHI HII INGEFIKA MBALI SANA NISHATI NA MADINI AWE DR IDRISSA .

    ReplyDelete
  5. Anayependa wananchi utaona matendo yake.
    Hongere Bkheressa .Ongea na Serikali isaidie Busara pale Bandarini Dar es salaam .Watu wanaopiga debe wawe na sare.
    Wapigadebe wengi wanawabughuzi Abiria haswa wakigeni na kusababisha waamuwe kupanda ndege kwa kuepuka kero.

    ReplyDelete
  6. magari 200, are you sure?

    ReplyDelete
  7. Hiyo "ferry" ina miaka mingapi tangu kutengezwa?

    ReplyDelete
  8. nini tofauti kati ya meli na kivuko?(ship and ferry/panton?)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...